Powered by RND
PodcastsGovernmentTANAPA PODCAST

TANAPA PODCAST

Tanzania National Parks (TANAPA)
TANAPA PODCAST
Latest episode

Available Episodes

5 of 16
  • TANAPA PODCAST EPISODE 14: MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI.
    Episodi hii inaangazia mila, desturi na tamaduni katika uhifadhi wa maliasili, hususan namna jamii ya Wangoni kutoka mkoani Ruvuma ilivyotumia majina na utamaduni wao kulinda Wanyamapori na Misitu  tangu enzi za mababu zetu.Hadithi hii ya kuvutia inaonesha jinsi urithi wa jadi ulivyokuwa chachu ya kulinda rasilimali za Taifa ambazo leo hii zinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya uhifadhi na utalii.Sikiliza simulizi hii adhimu kutoka kwa Chifu Songea Mbano wa Kwanza, kupitia TANAPA Podcast – Episode ya 14. Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaMgeni: Samweli Vitus Mbano (Chifu Songea Mbano I)Usikose kila Jumatatu na Alhamisi kupitia majukwaa mbalimbali ya TANAPA Podcast
    --------  
    55:20
  • TANAPA PODCAST EPISODE 13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili
    Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Katavi. Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika epsodi ya 13.Eneo: Hifadhi ya Taifa KataviMwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Wageni:1.⁠ ⁠Moses Edward Tende ( Mtemi Sigulu) Chifu wa Kabila la Wagongwe.2.⁠ ⁠Lukas Moses Msaga - Mtoto wa Mtemi Sigulu anayefundishwa kurithi mikoba ya Mtemi Sigulu.⁠3.⁠ ⁠⁠Askari Uhifadhi Daraja la Pili - Kimori Shiwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ikolojia, Hifadhi ya Taifa Katavi. Endelea kutufuatilia kupitia Platifomu za TANAPA Podcast.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
    --------  
    54:47
  • TANAPA PODCAST EPISODE 12 - Zoezi la Uhamishaji Tembo kutoka Misenyi kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato.
    Episodi hii imeangazia zoezi endelevu la kuwahamisha tembo walowezi kutoka maeneo ya karibu na wananchi kwenda hifadhini na zoezi zima la kuwaswaga tembo waliotoka hifadhini kuvamia maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini.Sikiliza Episodi hii kwa taarifa hiyo na mengine mengi kupitia Epsode ya 12.Eneo: Misenyi - Bukoba.Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaGuests: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Fredrick Mofulu - Mkuu wa Hifadhi Ibanda - Kyerwa. NaKamishna Msaidizi wa Uhifadhi Charles Ngendo - Mkuu wa Hifadhi Rumanyika - Karagwe.Fuatilia kupitia Platform za TANAPA Podcast.
    --------  
    50:02
  • TANAPA PODCAST EPISODE 11 - Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere na Historia ya Taifa letu.
    Kuelekea Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, TANAPA PODCAST tunakueletea uchambuzi kuhusu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Hapa utapata kujifunza mengi kuhusu harakati za Uhuru wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla.Ikumbukwe historia hii imehifadhiwa katika Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere iliyopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam. Fuatilia uhondo huo katika Epsode ya 11.Eneo: Dar es salaamHost: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaGuest: Afisa Mhifadhi Mkuu Mariam Njaritha - Mkuu wa Kituo Nyumba Kumbukizi ya Mwl. NyerereUsikose kila Jumatatu na Alhamisi kupitia Platform za TANAPA Podcast.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
    --------  
    41:52
  • TANAPA PODCAST EPISODE 10 - MAANDALIZI YA TWENZETU KILELENI 2025 NA PROF. KAMUZORA
    Episodi hii inaangazia mazungumzo ya kina kuhusu zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambapo Profesa Kamuzora anaeleza uzoefu wake katika kupanda mlima kwa muda mrefu.Fahamu faida ya kushiriki kampeni ya “Twenzetu Kileleni katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa Taifa letu, kuhamasisha utalii pamoja na utunzaji wa mazingira.Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano - TANAPAGuest: Prof. Faustin Kamuzora - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi UTT AMIS.
    --------  
    44:52

More Government podcasts

About TANAPA PODCAST

Karibu katika Podcast rasmi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), inayoangazia mazungumzo ya kina kuhusu Uhifadhi wa Maliasili zilizopo ndani ya Hifadhi za Taifa, Elimu ya Uhifadhi, Utalii pamoja na Fursa za Uwekezaji. Vipindi vya Podcast hii vinajadili mikakati ya uhifadhi endelevu, ukuaji wa utalii, na ushirikiano na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuhakikisha Rasilimali za Taifa zinatunzwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Podcast website

Listen to TANAPA PODCAST, The Law Show and many other podcasts from around the world with the radio.net app

Get the free radio.net app

  • Stations and podcasts to bookmark
  • Stream via Wi-Fi or Bluetooth
  • Supports Carplay & Android Auto
  • Many other app features
Social
v7.23.11 | © 2007-2025 radio.de GmbH
Generated: 11/8/2025 - 10:55:23 AM